WAYCAN Initiatives

Women And Youth Community Action Network Initiatives

WAYCAN INITIATIVES ni shirika linalojumuisha vijana na wanawake katika utenda kazi wake. Lilianzishwa na kusajiliwa kama Shirika Lisilo la kiserikali (NON GOVERNMENTAL ORGANIZATION) nchini Kenya mwaka wa 2013. Shirika la WAYCAN INITIATIVES linawalenga kama wahusika wakuu Wanawake na Vijana kwa malengo ya kueneza ufahamu wa Haki za Binadamu, kudumisha usalama, kuboresha maisha kiuchumi, na kuimarisha kujumuishwa kwa wanawake na vijana katika mipangilio na uongozi katika vitengo vya uongozi, utawala na kudumisha amani.

WAYCAN INITIATIVES inajitokeza kwa uzito zaidi kwa utumiaji wa mbinu bunifu zinazoshirikisha wanaolengwa na miradi yake na ambazo zinawavutia sana vijana. Mbinu hizi zina mizizi kutoka kwa sanaa shirikishi na zinaambatana kwa karibu zaidi na misingi ya kujieleza na tamaduni za ki-Afrika.

WAYCAN INITIATIVES ni shirika linalolenga, ki-msingi, kuboresha na kukuza ufahamu wa makundi mbali mbali ya kijamii katika nyanja tofauti tofauti zinazowahusu. Shirika la WAYCAN INITIATIVES linajivunia kuwa dogo na changa, hali ambayo inawezesha shirika la WAYCAN kufaulu kuwa na uhusiano wa karibu na makundi ya wahusika wanaofanya kazo nalo. Pia, hali hii inawezesha kutekeleza miradi inayowalenga vyema wahusika na kushughulikia mahitaji yao vilivyo, kwani shirika lina uzoefu wa kuelewa na kubadilisha mipangilio ya miradi ili iambatane na muktadha wa wahusika wanaolengwa na miradi yake. Shirika linaleta mbinu bunifu, shirikishi na pia ujuzi na ufahamu unaotokana na uzoefu wa kufanya kazi kwa muda mrefu wa maafisa wake. Wahusika wanasaidika na kushirikiana ili kutekeleza mbinu zilizojaribiwa na kufaulu mahali kwengine.

TUNAYOYAPATIA KIPAO MBELE HAPA WAYCAN INITIATIVES

Kupambana na hujuma za Itikadi Kali za kidini

Usawa wa Jinsia

Kuboresha Maisha Kiuchumi

Kutetea Haki zote za Binadamu

Kusuluhisha mafarakano na Kujenga Amani

Kuboresha Afya ya Jamii

Maono na Lengo Kuu

WAYCAN INITIATIVES ina maono ya maisha yanayowajumuisha wanawake na vijana katika maendeleo yao ya kudumu

Lengo kuu la WAYCAN INITIATIVES ni kupea kipao mbele na kusaidia kujumuishwa katika uongozi wa kutetea haki za binadamu, amani, siasa, usalama, utawala na maisha ya ki-uchumi ya vijana na wanawake, kupitia mbinu bunifu, zinazobadili fikra na tamaduni potovu.

Ofisi
Ofisi kuu ya WAYCAN INITIATIVES ipo Ukunda, kadiri mita 200 kutoka makutano ya barabara kuu ya Ukunda-Ramisi na barabara ndogo inayoelekea Diani Forest Lodge (Makutano karibu na ofisi ya Chifu wa Diani), Kaunti ya Kwale.

WAYCAN INITIATIVES pia ina ofisi ndogo ya kutafutia ufadhili wa miradi (Resource Mobilization Unit), jijini Nairobi katika mtaa wa Racecourse, katika barabara ya Ngong, karibu na Kevian Factory - ikiangaliana makaburi ya mashujaa wa vita vikuu vya dunia.

Maadili

Uwazi na Uwajibikaji

Heshima isiyobagua kwa wote

Usawa kwa nafasi za kujiendeleza

Hadhi na Haki.

Kushirikisha na kujumuisha wote bila ubaguzi wowote (dini, kabila, masomo ama hali ya kijamii)

MIRADI
Usalama

Miradi yetu inayolenga usalama katika jamii inafahamishwa na uzoefu wetu katika maswala ya itikadi kali, ambayo imedhihirisha kwamba, vijana wengi wanakutana kwa mara ya kwanza na maswala ya itikadi kali kwa bahati mbaya, au kupitia ushawishi wa wenzao, au kwa kulazimishwa na mara ingine kutokana na utundu au hali ya ujana kutaka kujua-jua mambo. Shida kuu ni kwamba jamii haina ufahamu au uwezo na mikakati ya kukinga na kutetea vijana kama hawa wanaokutana na makundi haramu, na walio katika athari kuu ya kushawishiwa kuingia makundi ya kigaidi. ... endelea

Haki za Binadamu na Usawa wa Kijinsia
Haki za Binadamu ndio msingi mkuu wa usalama na kutengamana. WAYCAN inatekeleza ki-makusudi miradi inayoongeza uwezo wa jamii, hasa vijana na wanawake kufahamu na kutetea haki za binadamu. Usawa wa ki-jinsia unadumishwa katika miradi na hata katika jinsi WAYCAN inavyotenda kazi na katika uteuzi wa maafisa wake. endelea
Maisha Kiuchumi
Tunaamini kwamba wanawake ndio "wanaoshona nyuzi za uhusiano katika jamii" kwa hivyo kupea wanawake ujuzi na uwezo wa kiuchumi inainua jamii kwa jumla. Vijana nao wanaathirika zaidi wakikosa kitu cha kufanya kinachoweza waletea mapato. Miradi ya WAYCAN inalolenga kuboresha maisha ya kiuchumi hutoa mafundisho ya kibiashara, kujenga mifano hai ya kuiga na pia kutoa mawaidha na usaidizi wa kibiashara. endelea
WASILIANA NASI
Unahitaji kujua zaidi? Wasiliana nasi kupitia:
 • UNAVYOWEZA KUWASILIANA NA WAYCAN INITIATIVES

  barua pepe: info@waycan.org

  Simu : +254 727 300 018 and +254 718 765 075

  Ofisi ipo
  umbali wa kadri mita 200 kutoka makutano ya barabara kuu ya Ukunda-Ramisi na barabara inayoelekea Diani Forest Lodge,
  Ukunda - Kaunti ya Kwale